PATANISHO: Mama mkwe anataka kunipiga ili kulipiza kisasi

Mwanadada kwa jina Roslyn, 28, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke mwenza Rosemary, 37.
"Nilienda kwake Disemba mwaka uliopita na akanikaribisha vyema naye akaja kwangu Januari na nikamkaribisha vyema lakini alikuja na vita. Sasa nikamwambia sielewi mbona alileta vita lakini nikamwambia afanye anachotaka.

Hapo bwanangu akamtafutia fedha na akarudi kwao." Alielezea Roslyn.

Aliongeza:

Sasa mtoto wa Rosemary alikuja kutembea na alikuwa na tabia mbaya. Mara alikuwa anapiga kelele mara anapekua pekua begi zangu na nikimkelelesha ananiongelesha vibaya akiniuliza kama mimi ni mamake. Hapo nikakasirika na nikampiga vibaya sana.

Kumbe huyu msichana alimpigia mamake na akanitishia kuwa atasafiri hadi Nairobi kulipiza kisasi.

Rosemary ameolewa kwa miaka kumi na mmoja huku Roslyn akiwa ameolewa kwa mwaka mmoja.

Alipopigiwa simu bi Rosemary alikiri kuwa amemsamehe Roslyn lakini anafaa kujua kuwa Albert mume wao ana bibi na watoto wengine na anafaa kuwakubali.

"Mimi nimekusamehe lakini unafaa kujua Albert ana mke na watoto wengine na nilichokuambia ni kuwa nilikuwa tayari kupigana nawe, hiyo nyumba ingekuwa imewaka moto."Alisema.

&t=1s