PATANISHO: Mama yangu alimrushia mama mkwe cheche za matusi

Bi, Beatrice alituma ujumbe akisema kuwa walikosana na mamake miezi miwili iliyopita juu ya ndoa yake akisema kuwa mama alimtusi mumewe.
Mama mkwe alikuwa anatoka western akija Nairobi na mamangu aliposkia alifikiria ni kama wanataka kunichukua wanipeleke ushago, hapo mamangu akampigia mume wangu simu akamtusi akiwakanya kuwa wasijaribu kunipeleka kwao. Alisema Beatrice.

Aliongeza,

Baada ya hayo bado alimtusi mume wangu akisema kuwa asiwahi fikiria kwenda kwetu nyumbani na pia mimi akanikanya, na kwa kuwa alikuwa amenitafutia kazi nyumbani alisema pia mimi nisikanyange kule.

Mume wangu tulikosana baada ya kumfumania na rafiki yangu lakini sio eti niliwapata wakifanya jambo mbaya. Hapo tukagombana na nikatoka na kwenda kwa dadangu kwa wiki moja.

Anasema kuwa alipomueleza dadake kila kitu naye akampelekea mamake mushene na hapo mama akakasirika vibaya na akaleta uzozo huo wote.

Beatrice alisisitiza kuwa yeye hana shida yoyote na mama mkwe kwani wana uhusiano mwema.

Mama Njeri, alipopigiwa simu alisema kuwa amekuwa akingoja mwanawe na mumewe waje nyumbani waombe msamaha akisema kuwa hao ndio wenye makosa.

"Mnajua mimi ni mtu wa kukasirika haraka mbona mliniambia maneno yenyu?" Aliuliza mama Njeri kabla ya kukiri kuwa amewasamehe kwa roho moja.