PATANISHO: Mamangu alituwacha na kutowekea Mombasa

Bi Sheila alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mamake mzazi ambaye alitorokea maeneo ya Mombasa.

'2014 alituwaha tu, tuko watatu kwetu nami nina umri wa miaka 19 na ndugu yangu ana miaka mitatu huku mdogo akiwa na mwaka mmoja. Mamangu alituwacha miaka minne sasa na akaenda Mombasa.' Alieleza Sheila.

Nilijaribu kumtafuta mamangu kupitia simu na kwa hasira nikamtusi nikidai sina mama na kuwa alifariki. Kwa hasira alidai nisiwahi mpigia simu na kuwa hata akifariki nisiwahi kanyanga kwa matanga yake, mimi nilikuwa nataka hata akifariki afariki na amani asiniwachie laana." Aliongeza.

Juhudi zetu za kumtafuta mamake Sheila hazikufua dafu.