PATANISHO: Marafiki wa mume wangu walifichua kuwa ana mke mwingine

Bi Rebecca alituma ujumbe akidai yeye na mumewe bwana Gitau, wamekosana baada yake kumpiga vibaya lakini licha ya hayo bado angependa kupatanishwa

"Hatukuwa tumekosania chochote lakini alikuwa ameenda na mwanamke mwingine ulevi na aliporudi mtoto wetu alikuwa mgonjwa na dawa aliyomeza ilimfanya atapike." Alieleza mwanadada.

Aliongeza,

Sasa mume wangu alipopata akitapika akadai sijampa mtoto chakula na nilipojaribu kumuelezea akanirushia cheche za matusi. Hapo nikamuomba asinitusi mbele ya watoto na akakasirika na kunigonga mangumi ya macho na hiyo sio mara yake ya kwanza"

Wawili hawa wamekuwa kwa ndoa ya miaka 16 na isitoshe mumewe ana mke wa pili ambaye bado hamtambui.

Alipopigiwa simu bwana Gitau alikiri kuwa alikasirika baada ya mkewe kumtusi na hapo akamgonga na hapo akamuomba msamaha.

"Nampenda kwani sina mwingine na hata huyo Wambui simjui." Alisema bwana Gitau.

Rebecca alikiri kuwa marafiki wa Gitau walimwambia huenda anapigwa na mumewe kwa sababu kuna mwanadada mwingine kwa jina Wambui.