PATANISHO: Mimi na dadangu tulimvuraga mume wangu na kumraruria nguo

Mama Precious aliomba apatanishwe na mumewe bwana Simon akidai kuwa alimfanyia maovu sana na akamwambia kuwa hatawahi pata mume mwingine.

Alisimulia,

"Nilitoka kwa mume wangu na kurudi shule na akinipata nikitoka shuleni anawavamia wenzangu kwani nilikuwa mixed school. Kuna siku alikuja kwetu na kuniambia kuwa nina tabia za umalaya na kwa hasira mimi na dadangu mdogo tukamshambulia.

Tulimtandika hadi tukamrarua manguo mpaka akashindwa kutembea na tulipoona watu wakitembea tukapiga mayoye tukisema ni mwizi. Watu walianza kumpiga na karibu wamuue."

Mama Precious anakiri kuwa amejaribu kutafuta bwana kote kote na amekosa mwingine huku akiamini kuwa amerogwa. Anasisitiza kuwa anataka kurudiana naye kwani yeye ndiye baba wa watoto wake.

Simon alipopigiwa alisema,

Nilikuambia tutaketi chini tuongee kwani ulinikosea sana. Vile ulirudi shule tulikubaliana vyema na ile siku nilikuja kwenyu uliniita hadi mwizi." Alisema Simon akisema kuwa alioa na hawezi oa wanawake wawili lakini atamshughulikia mwanawe.

Hata hivyo, mwishowe wawili hao walisameheana lakini Simon akasisitiza kuwa hawezi rudiana na mama Precious.