patanisho

PATANISHO: Mimi Nampenda Mume Wangu Heri Hata Niende Kwake Aniue

Karen mwenye umri wa miaka 22, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe Peter.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya mwaka mmoja na hawajajaliwa mtoto bado.

PATANISHO: Raphael Abubujikwa Na Machozi Baada Ya Mkewe Kutoweka

Kulingana na Karen; “Tulikosana mnamo tarehe 22 mwezi wa saba. Mimi tulivyooana na mume wangu aliniwacha nyumbani na mama mkwe naye akasafiri kikazi hadi Ngong. Juzi tukakosana na mama mkwe na nikampigia mume wangu simu kumueleza kuwa nilihitaji nauli ili nisafiri hadi nyumbani.

Alinitumia na niliposafiri nikarudi baada ya siku kadhaa lakini mama mkwe akanikanya kufika katika boma lake na hapo nikasafiri hadi kwa ndugu yangu.”Alieleza bi Karen huku akifichua kuwa kuna mwanadada fulani aliyempigia simu akidai kuwa ni mpenzi wa bwana yake.

Basi nilimpigia bwanangu kumuuliza kuhusu hayo na akakiri kuwa yule ni mpenzi wake sasa nashindwa ni nini nilimfanyia na vile nampenda.

Mimi nampenda bwanangu na hata akinikataa nitaelekea hadi kwake aniue heri hata nilale kwa mlango. Mimi nampenda sana bwanangu.” Alisema.

PATANISHO: Sijui Mbona Kijana Ana Uwoga Wa Kumuendea Mkewe Nyumbani

“Unajua kwa hii dunia kitu kibaya ni kuoa mwanamke halafu atusi mama mzazi.” Alidai Peter.

Unajua hata miezi mitatu haijapita tangia baba mzazi alifariki na hata machozi hayajaisha na mke wangu amemtusi.” Alieleza akisisitiza kuwa bado anampenda mkewe na anafahamu kuwa mkewe anampenda.

Mimi nakupenda sana kwani wewe ndio bwanangu milele!” Alisema Karen huku akisema kuwa atarekebisha tabia zinazoudhi familia ya bwanake.

PATANISHO: Mume Wangu Alitaka Kukimbia Na Mtoto Hadi Rwanda

Pata uhondo kamili.

Photo Credits: victor TKO imboto

Read More:

Comments

comments