patanisho.reloaded

PATANISHO: Mimi Ni Mluhya Siwezi Ishi Bila Bibi!

Eunice aliomba apatanishwe na mumewe ambaye walikosana takriban wiki tatu zilizopita.

Kulingana na Eunice, 27; “Nimeishi na huyo mume kwa miaka tisa na tukajaliwa watoto wanne. Baada ya kujifungua mtoto wa nne hapo ndipo mambo ya kukosana kwa nyumba yalianzia, hakuwa ananisaidia kwa mambo ya nyumbani na nilikuwa naenda kwa mama mzazi kuomba usaidizi.

PATANISHO: ‘Sisi Kama Wana Marogoli Hatupendi Ujinga, Hatubembelezi Watu’

Hapo mamangu akaniarifu niende nikaishi na dadangu ili nipunguze mawazo na pindi tu nilipotoka, bwanangu alibomoa nyumba yetu na kuchoma kila kitu kwa nyumba na kuniarifu kuwa nisitarajie kuna chochote changu,” alieleza Eunice.

Alipopigiwa simu bwana Fredrick, alifuruhishwa sana kuskia sauti ya bwana Gidi na Mulee huku akidhani ni kitengo cha kujishindia pesa.

“Namjua Eunice,” alisema bwana Fredrick mwenye umri wa miaka 29.

“Meli iking’oa nanga haina breki hadi mwisho. Mimi kama mtu mzima mimi ni mchungaji. Maandiko yanasema mwanamke mjinga hubomoa nyumba yake kwa mikono miwili. Hakuna vile mwanamke anaweza tusi mamangu na kisha aishi kule,” alijitetea Kimathi.

PATANISHO: Kakangu Alimkashifu Dada Yetu Kuwa Ni Illuminati Na Alimuua Ndugu Yetu

Sasa kama anasema sikuwa namshughulikia, mwenye alikuwa anamshughulikia na watoto awapeleke kwake basi. Usijaribu kunipigia simu siku nyingine nimejaribu kukuambia huskii, wewe endelea na maisha yako na maisha yaendelee,” alisema akifichua kuwa yeye tayari amefunga ndoa na mwanamke mwingine kwani kama Mluhya hamna jinsi anavyoweza ishi pekee yake.

Pata uhondo kamili.

Photo Credits: victor TKO imboto

Read More:

Comments

comments