PATANISHO: Mimi PA Wa Mheshimiwa nanyang'anywa aje mke na mtu wa bodaboda?

gidi.na.ghost.patanisho
gidi.na.ghost.patanisho
Bwana Dino alituma ujumbe akidai kuwa kuna jamaa wa bodaboda ambaye anamharibia ndoa yake ya miaka saba.

"My brother nimeishi na mke wangu kwa miaka saba na sijawahi mguza hata kofi. Kuna siku kulikuwa na mambo ya mazishi kwao na nikamruhusu aende. From there kuna jamaa wa bodaboda ambaye alikuwa anambeba wanaenda town kufanya maneno yao." Alieleza Dino.

Sasa baada ya kutizama fainali ya Ufaransa nikampata huyo jamaa nikamweleza nataka tuzungumze maneno kadha wa kadha afisini mwangu.

Sasa nikapata amemtumia mke wangu ujumbe akiuliza afanye nini atakapokutana nami, hapo mke wangu akamweleza aruke futi mia moja, kuuliza mke wangu alikubali alikuwa na uhusiano na huyo jamaa. " Aliongeza huku akiwa na wingi wa hasira.

Kilichomkasirisha Dino ambaye pamoja na mkewe wamejaliwa watoto wawili, ni kuwa yeye kama mwalimu na msaidizi wa mheshimiwa ana pokonywa mke.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be