PATANISHO: Mke wake alikuwa anamaliza gorogoro mzima kama jini

ugali.1
ugali.1
Leo ikiwa Jumatano ya kwanza mwezi huu wa machi, aliyeomba kupatanishwa ni bwana James.

Aliomba apatanishwe na mamake mzazi akidai walikosana miaka miwili iliyopita baada ya kufanya mkewe wa miaka 15 kutoroka nyumbani na isitoshe hataki kuwaona wajukuu wake 5.

"Tumekaa hadi na wajomba ili tusuluhishe lakini bado hatuelewani na chanzo kilikuwa mke wangu ambaye tumekuwa kwa ndoa ya miaka 15 na tangia aondoke imekuwa miaka mitano." Alieleza James.

Aliongeza,

Aliniambia nitumie fare siwezi kaa na mamako na nisipotuma atatembea miguu hadi Eldoret. Babangu pia alimkalisha mamangu chini kutaka kujua mbona anawachukia wanawake kwa boma letu."

James anasema angependa amuombe mamake msamaha kwani tangia wakosane na mke wake hajawahi kuwa na amani na pia kazi yake haijakuwa sawa.

Bwana James anateta akisema ni kama mama yao hatambui wana wake wengine akisema,

"Mimi nikasafiri hadi nyumbani siwezi chinjiwa kuku na huyu mtoto mwingine anafanyiwa kila kitu na eti sisi wote ni wana wake."

"Huyu mtoto nampenda sana lakini alifika wakti akaanza kunitusi na nilipoona ameanza kuchanganikiwa nikawacha kuzungumza naye." Alisema mama James.

Aliendelea akisema mwanawe alimwambia, "Alinitusi akisema kunywa maziwa ya watoto wako wanaofuga ng'ombe unone matako!"

Isitoshe mamake James anasema kuwa mwanawe alikuwa na tabia ya kumsingizia kuwa alikuwa anakula chakula kingi kwa boma ila ilikuwa mkewe.

"Mke wake alikuwa anamaliza gorogoro mzima kama jini!"