PATANISHO: Mke wangu alianza tabia za mipango ya kando nilipoelekea kazini

Bwana Kitur alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Carol, ambaye alitoweka nyumbani majuma mawili yaliyopita.

"Hakuna kitu nilimfanyia, mimi ndio nilienda kazi pande za Eldoret mwaka jana. Na nikiwa kazini nikaskia fununu kuwa ana mipango ya kando, huku akienda kwa bar na kubugia pombe.

Sasa nikasema haya maneno ya watu lazima nidhibitishe. Wiki tatu zilizopita nikarudi nyumbani bila kumwarifu na sikumpata ila watoto walikuwa nyumbani. Asubuhi mida ya saa kumi na moja na dakika thelathini na sita nikaona pikipiki akifika sasa." Alieleza bwana Kitur.

Sasa nikashindwa huyu ni mwanamke wa aina gani. Akabisha mlango na kuita mtoto, alipoingia akanipata nimeketi kwa kiti. Akaanza kutetemeka na kuangusha simu. Kumuuliza alipokuwa akaomba msamaha na nikampiga." Aliongeza akidai kuwa wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na mitatu.

Alisema kuwa mkewe alidai kuwa yeye huchelewa kurudi nyumbani na kuwa hawezi vumilia kwa mwezi mmoja.

Alipopigiwa simu, Carol alimlaumu mumewe kwa kwenda kazini na kukaa huko na kumwachia watoto pekee yake.

"Nilikuwa nafunga kazi saa tatu na kuna watu walikuwa wanamwambia maneno tu. Na hakunifungulia ile kazi ni mimi mwenyewe kwani lazima ningelisha watoto." Alieleza.

Pata uhondo kamili.