patanisho

Patanisho: Mke Wangu Alidai Kuwa Haja Yake Ni Kula Fedha Za Wanaume Wengine

Bwana Joseph alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi, Susan akiomba msaada kwani anapitia maisha magumu.

“Mwaka uliopita tulikosana na mke wangu kidogo na akatoweka akarudi nyumbani. Sasa wazazi wake wakaona anapitia maisha magumu na wakamrudisha Nairobi. Nikamweleza aje nyumbani tulee watoto wetu.

Sasa aliporudi shida kuu ilikuwa tabia ya kuongea na wanaume wengine usiku wa manane tukiwa na yeye kitandani. Nikimuuliza anadai kuwa hawataki ila anataka tu kula fedha zao.” Alieleza Joseph.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minne na wamejaliwa na watoto wawili.

Susan ambaye ni shabiki wa Radio Jambo hakutaka kuzungumza nasi.

Pata uhondo kamili.

Photo Credits: victor TKO imboto

Read More:

Comments

comments