patanisho.

PATANISHO: Mpenzi wangu alimwagia maji na jivu kitandani mwangu

Samson na mpenzi wake bi Joyce, waliyekosana jumamosi iliyopita, akisema kuwa amemfanyia maneno, alimwagia maji na jivu kitandani, akakatakata nguo zake kisha kuondoka.

Ilikuwaje; Pasta Ng’ang’a aeleza jinsi alivyojizolea wafuasi Kanisani mwake

“Bwana wanaume wanapitia tabu Jumamosi nilidhani nimepata kumbe nimepatwa. Nilitoka na akaniambia nimwachie fedha za chakula na nikamwachia.

Kurudi nyumbani nikapata amefunga mlango na kuulizia nikaambiwa anarudi na jumapili nikitaka kwenda kanisani nikapata amekata kata zote. Kujaribu kumtafuta na simu hakushika simu.”

Anasema kuwa mkewe alipanda gari iliyoleta maiti na ilikuwa inarudi Nairobi na anashuku yuko Nairobi kwa sasa.

Wawili hao wamekuwa kwa uhusiano wa miezi minne baada ya wawili hao kuzungumza na dadake na kuelewana.

“Huyu jamaa tulipatana mwaka ulioisha na tukaelewana kama atajenga nyumba nitaishi naye na akajenga na tukaoana. Lakini jamaa alianza kuskiza watu na kunitusi na akanitusi akisema kuwa atanifukuza na nirudi kwetu.” Alieleza Joyce akidai kuwa mumewe hakutaka aende kwa wanadada zake.

Anasema kuwa alikata nguo zake kidogo na akaambia mamake kuwa hawezi ishi naye na kwa hayo hayuko tayari kurudiana naye na atarudi baada ya mwaka mmoja.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments