PATANISHO: Mke wangu aliniambia ameolewa niachane naye

Leo katika kipindi cha patanisho mwanamume mmoja ambaye alijitambulisha kama Alphonse Kimanthi alituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake Jackline ambaye walikosana mwaka jana machi.

Kimanthi alisema kuwa akitoka kazini alikuwa anarudi nyumbani na kumpata amenuna kila siku.

"Kila mara nilikuwa narudi nyumbani na kumpata mke wangu amenuna,siku moja nilipata kazi ya kuenda Kibwezi kuamka asubuhi alinipa matusi hadi akanitusi na wazazi wangu na ndugu zangu

Nilikasirika nikamchapa makofi mawili, kurudi kutoka kazini nikapata amekusanya virago na kuenda, tulikuwa tunazungumza naye tangu siku hiyo hadi mwaka jana Desemba

Niliwatumia pesa za sikukuu, huu mwaka Juni,23, kumpigia simu aliniambia nisiwahi mpigia simu kwa maana ameolewa." Kimanthi Alieleza.

Kimanthi alipoulizwa kiini chao cha kukosana alikuwa na haya ya kusema,

"Ni kama mke wangu alikuwa na mpango wa kando kwa maana kuna siku usiku alipigiwa simu kumuuliza akaniambia nisimsumbue  , tumekaa na mke wangu kwa muda wa miaka saba

Baada ya hapo alinipa namba ya simu ya mwanamume mwingine akaniambia ameolewa naye, kumpigia simu huyo mwanamume alianza kunitusi."

Baada ya Jackline kupigiwa simu alikata simu na kukana kuzungumza.

Kwa mengi zaidi tembelea mitandao yetu ya youtube.