PATANISHO: Mke wangu aliniambia atanitesa kwa miaka kumi

Bwana William aliomba apatanishwe na mkewe wa miaka ishirini ambaye walikosana mwaka jana.
"Tumeishi na yeye kwani nilimuoa akiwa mdogo baada yake kumaliza kidato cha nne. Tumejaliwa watoto watatu ambao wako shuleni."Alisema William.

Sasa tumeishi na amani na hatujawahi kosana naye halafu nikaskia 2017 mwezi wa nne wakati walikuwa wanaandika wanajeshi. Sasa mkora alitoka Nairobi akaja akamweleza naandika watu kazi na akaambiwa atafutiwe watu watatu kazi.

Sasa mke wangu akatafuta watatu ambao walitoa elfu mia tatu kwa kila mtu na akapatia huyo jamaa. Lakini mke wangu hakunijulisha kuna mpango anafanya pale kwa miezi minane na kuna watu walikuja kunitafuta wakidai fedha.

Sasa tulikosana na mke wangu na huwa tunazungumza naye saa zingine anacheka na kuna siku aliniambia atanitesa miaka kumi kwani sahii yuko raha." Alieleza William.

Alipopigiwa simu bi Mary alisisitiza kuwa atampa mke wake kichapo cha miaka kumi.

"Character zake ndio zilinikasirisha. Alikuambia ana mwanamke? NIlimsamehe alipo zaa mtoto mmoja nje ya ndoa sasa ya pili akarudia. Halafu kilicho nichosha zaidi ni nililea watoto niliompata nao hadi wakamaliza shule lakini wangu hakuwa anataka kuwaona." Alijieleza.

Pata uhondo kamili.