PATANISHO: Mke wangu alinianza madharau nilipo poteza kazi

Sammy kutoka kitengela alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe ambaye anadai walikosana pindi tu kazi yake ilipoisha, kwani hapo ndipo madharau kutoka kwa mkewe yalipoanzia.

"Nilipoteza kazi yangu last year but one na hapo ndio madharau ilianza kutoka kwa mke wangu. Nilianza kufanya kazi ya barabara kama dereva.

Nikimuuliza kwenye kitu kiko yeye huniuliza namuuliza kama nani na kuwa nafaa kutafuta kazi ili aniheshimu kama mwanaume." Alieleza Sammy.

Wawili hao wameoana kwa miaka mitano na wamejaliwa mtoto wa miezi saba.

Isitoshe, Sammy anasema kuwa mazungumzo kati yao yamedorora na leo asubuhi aliamka na kwenda safari bila kusema alikotoka.

Sammy anadai kuwa aliposhika simu yake siku moja, alipata ujumbe kutoka kwa wanaume wakimtongoza na alipo ongelesha mmoja wao, alikiri kuwa mkewe hajawahi sema kuwa ameolewa.

Hata hivyo juhudi za kumpata mkewe hazikufua dafu.