PATANISHO: Mke Wangu Alinichomea Kazini, Nilikuwa Jeshi Sasa Mimi Ni Hawker

16649565_647102085477744_6951482243422551022_n
16649565_647102085477744_6951482243422551022_n
Bwana Joseph alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Alice.

Alisema kuwa wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na miwili na wamejaaliwa watoto watatu.

"Mimi nilikuwa afisi wa jeshi, niliajiriwa mwaka wa 2003 na nikaoa mwaka uliofuata maeneo ya Eldoret. Kazi ya jeshi ni kuhamishwa hamishwa na wakati huo nilikuwa naishi Marigat mahala ambapo hapakuwa na network nzuri.

Sasa katika hiyo hali mke wangu nilikuwa na muachia hadi ATM ashughulikie watoto. Sasa nisiporudi jioni anapigia wakubwa wangu au anakuja hadi kambi kusema kuwa hajaniona kwa mda flani. Wakati mmoja aliniripoti kwa mkubwa wangu akidai kuwa ananishuku kuwa nina mwanamke mwingine na niliporudi kutoka kazini niligombezwa na wakubwa.

Hapo nikamkanya kwani alikuwa ananiaibisha lakini hakukoma." Alieleza Joseph akidai kuwa baada ya yale, jina lake liliharibiwa na wakubwa wake hawakuwa wanamheshimu.

Mimi niliwacha kazi kiasi bila ruhusa na baada ya yale nilifungwa na nikawachiliwa na nikawachishwa kazi. Aliongeza jamaa huyo ambaye sasa hivi anafanya kazi ya uchuuzi.

Alipopigiwa simu bi Alice alisema kuwa hana mda wa kuzungumza kabla ya kukata mawasiliano.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be