PATANISHO: Mke wangu alinikasirika baada ya kumwambia afike nyumbani mapema

Bwana Baraza alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe ambaye walikosana baada ya mkewe kuanza kufika nyumbani akiwa amechelewa.

Baraza alisimulia,

Ilikuwa last Saturday wakati niliingia nyumbani kutoka kazini na kama kawaida najua mke wangu hufika nyumbani 8:30, sasa ikafika 8:3opm simuoniilipofika saa nne nikaanza kujiuliza mbona hajafika.

Sasa nikaamua kwenda kumtafuta kwani najua kwenye anafanyia kazi. Kitu ikaniambia nirudi kwa nyumba na nilipofika nyumbani nikapata akila kile chakula nilitayarisha na hakuwa anazungumza nami.

Aliongeza,

Niliona kwa ile hasira nisimuulize chochote nikangoja hadi asubuhi na aliniambia kuwa alibadilisha kazi na nisimuulize maneno ya masaa. Aliniambia kama tutaongea maneno ya masaa heri tutengane. Sasa nikatoka nikaelekea kazini na nikasema nikirudi nyumbani tutazungumza na kama nimemkosea anisamehe.

Sasa kurudi nyumbani nilipata amefunganya virago vyake na kuondoka na kuwacha watoto wetu nyumbani.

Alipopigiwa simu bi Jackline alidai kuwa wawili hao wameihsi kwa miaka kumi na mitano na bwanake alianza kumsumbua na kumtesa akiwa na mimba ya miezi mitano.

Upande wa masaa, yenyewe mimi ni salonist na utanipata nikifanya hiyo kazi hayo masaa. Ubaya wa mume wangu hudhania namchezea akili na kuwa nina mipango ya kando." Alieleza Jackline.

Pata uhondo kamili.