ghostandgidi

Patanisho: Mke wangu alinipiga ngumi kama ya GSU

Tulianza rasmi kitengo cha patanisho na yule aliyeomba patanisho ni Kirinya aliyetuma SMS kwa Gidi huku akisema ndoa yake iko karibu kusambaratika akongeza ‘my wife Wangari is not talking to me help me please please.

Doh, kisa na maana. Bwana Kirinya alimwelezea Gidi kilichotendeka

‘Mimi nampigia simu kuna wakati aliniambia anataka kwenda kwao nyumbani na watot ashapeleka huko nimpatie fare. Unajua mimi ni driver wa shule. nikamwambia nitapitia kwake kazi nimpatie pesa an viatu nilinunulia watoto. Kupitia huko nikapata nimwekwa blacklist hata jana nilikuwa nimempigia akaniambia nisiwahi mpigia tena akaniweka mpaka kwa blacklist hata leo sikuenda kazi nione kama mnaweza kunisaidia. 

Mbona Bibi yake Wangari alikuwa amepeleka watoto ushago hapo awali?

Bwana Kirnya alimwelezea, ‘Unajua yeye alisema watot huku ni shida mimi niakmwabia angoje nipeleke numbai kwetu alikataa akaniambia anataka kupeleka watot kwao mimi nikamwambia wapeleke tuu mimi sina shida nitakuwa natoa pesa ya shule na kila kitu Heh naye alinipiga ngumi kama ya GSU bwana. 

Kwa hivi sasa, mke wake Wangari ako wapi?

‘Yeye ako kazi lakini mimi niko nyumbani leo sikuenda kazi Akitoka kazini anarudi nyumbani. Mimi naona hii ndoa ikeinda kuenda tuu. 

Licha ya haya yote Kirinya bado angependa kurejesha uhusiano kati yake na Wangari.

Kirinya ana miaka 32 na Wangari ni 28 na wamebarikiwa na watoto wawili. Ndoa wamekaa kwa miaka nne.

Wangari aliweza kushika simu ya Gidi na kufichua kama yeye ‘si kichwa ngumu’ na mengineo kwa ufupi.

‘Ati mimi ni kchwa ngumu. Sasa nikuulize Gidi, kama hajawahi nipeleka nyumbani kwao na ni kama hajinitambua rasmi kama mke wake’.

Ombai langu ni anipeleke kwao na apange safari nitambulike rasmi.

Skiza kanda usikie maneno matamu kati ha hawa wawili

 

 

 

 

Photo Credits: radiojambokenya

Read More:

Comments

comments