PATANISHO: Mke wangu alinisingizia kuwa nimepachika mtoto mimba

Paul kutoka Bondo na mkewe bi Achieng', akisema amesombwa mawazo mengi sana.

Alisimulia,

Soma haya:

Mimi ni mzazi na nina watoto wanne na mke wangu wa miaka kumi na minne. Chenye iko  ni eti tuna wasichana wawili ambao sasa wamekuwa wakubwa. 

Wasichana hawa wana tabia ambazo hazinifurahishi kwani nikitoa masharti mama anaona nikama nawasumbua ni kama mimi sio baba yao. Mmoja wao aliteleza na akapata mimba.

Nikamwambia sasa uulikuwa unataka mimba sana na sasa utajua majukumu yake, kumbe yeye na mama walinipangia njama wakidai kuwa ni mtoto wa dada yangu.

Paul alisema kuwa ilikuwa porojo ili waharibu jina la mtoto wa dadake lakini mimba ililikuwa ya jamaa fulani wa kando na walijua kuwa angemshtaki.

Isitoshe mwanawe ambaye ako darasa la saba pia alipachikwa mimba na kwa hasira bwana Paul alivunja vunja nyumba aliyomjengea mkewe.

"Si wewe ndio ulitangaza kuwa nikija huko utaniua mara utaua mtoto, si ulisema hivo?" Aliuliza Achieng akidai kuwa hana shida ya kurudiana na bwana Paul lakini kwanza amtumie nauli.