PATANISHO: Mke wangu alinitenga alipogundua natongoza mwanafunzi

Bwana Mark alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe mama Pesh akidai hana amani.
"Kuna wakati tulikuwa tunaishi maeneo ya Kitale na kuna wakati alinipata na msichana tukiwa tunatembea naye, mwanafunzi jirani na hapo alikasirika.

Nilikuwa namtongoza lakini hatukuwa tumefanya lolote naye." Alikiri bwana Mark.

Bwana Mark ana miaka 25 huku mkewe akiwa na miaka 22 na wawili hao wana watoto wawili.

Alipopigiwa simu mama Pesh alidai kuwa walikosania mambo kidogo kidogo ya nyumba na ilifika mahali akachoka.

"Alikuwa akinipiga sana na bado akaanza mipango ya kando kinyume na chenye nilikuwa nimemfanyia kwani nilikuwa nampenda kama mume wangu." Alieleza Pesh.

Niliwapata na huyo msichana wakiwa wanazungumza na huyo msichana alikuwa na sifa mbaya na isitoshe alikuwa rafiki yangu. Isitoshe yule Rozie alidai kuwa hamuachi mume wangu na hapo nikaamua kujipa shughuli." Alifichua Pesh.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be