gidi.ghost.patanisho

PATANISHO: Mke wangu aliondoka na kusema watoto wetu wanaweza ishi kama yatima

Vincent alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe wa miaka mitano, Bi Lydia ambaye hivi majuzi aliamua kufunga virago na kuondoka nyumbani kwao na kumuachia watoto watatu.

Patanisho: Nilitoweka Kwangu Na Kumuacha Mke Wangu Na Mtoto

 

“Hatukuwa tumekosana. Mimi nilikuwa nimeelekea kazini na nikapigiwa simu kuelezwa kuwa mke wangu amefunganya virago na kuondoka.

Kumpigia simu mamake alinitusi sana akidai kuwa nilimtesea mtoto kwani kazi yangu ni kukaa tu nyumbani na kula fedha za mke wangu.” Alieleza Vincent akidai kuwa mkewe alimueleza kuwa atafute mke mwingine ambaye atalea wanawe.

 

Patanisho: Mke Wangu Alidai Kuwa Haja Yake Ni Kula Fedha Za Wanaume Wengine

Alipopigiwa simu bi Lydia, alidai kuwa mumewe alimtesa sana na hata bado hajamuoa ki rasmi na kuwa hataki lolote kumhusu.

“Mimi nafanya kazi yeye hushinda tu ameketi na akipata fedha kiasi hushinda ame bet bila usaidizi wowote. Isitoshe kazi ni kunitusi kwa simu akiniita majina yote.” Alidai Lydia.

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments