Patanisho: Mke wangu alipachikwa mimba na mpango wa kando

Bwana Otieno aliyekiri kuwa mkewe bi Betty, alienda nje ya ndoa, alituma ujumbe akiomba apatanishwe. Isitoshe, katika harakati ya mipango ya kando alipachikwa mimba.

"Mke wangu alienda nje ya ndoa na nikagundua kuwa ana mimba ya yule mpenzi wake. Kisa hicho kilinikasirisha na niliondoka na kwenda akiwa miezi kadhaa kabla hajajifungua." Alieleza Otieno akisema anataka apatanishwe na mkewe huku akidai aligundua kuwa haoni kama atapata mke mwingine kama yeye.

Otieno alifichua kuwa wawili hao waliingia kwa ndoa huku mkewe akiwa na watoto watatu tayari.

Mke wangu alikuja akanidokezea kuwa mkewe alidanganywa na msichana wa kazi aende nje ya ndoa.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitano.

Betty alipo ombwa msamaha alikiri kuwa hana shida kwani yuko tayari kurudiana na mumewe.

"Ni sawa sina shida wacha nishughulike mambo na watoto shule tutaongea." Alisema Betty akiongeza, Sina shida naye tumesameheana."

Cha kushangaza ni kuwa Betty alisema kuwa mimba ni ya Otieno na kuwa aliyemdanganya mimba sio yake ni kama alikuwa na nia ya kumuoa. Swala hilo lilimfurahisha mumewe Otieno.

Pata uhondo kamili.