PATANISHO: Mke wangu alipigana na mamangu mzazi

Bwana Duncan Kaka alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Mary akidai wawili hao walikosana juma moja lililopita, huku akiongeza jambo hilo linamyima amani.

"Tulikosana na mke wangu last week na akakasirika na kufunganya virago na kuondoka." Alisema Duncan. Tulikuwa nyumbani kwa msimu wa krisimasi na kabla ya hayo alikuwa amekosana na mama mkwe na wakapigana na kuishi kwa takriban mwaka mmoja bila kuzungumza.

Hayo tukasuluhisha lakini nikamueleza kuwa tunafaa kwenda nyumbani ili akaombe msamaha. Alikataa kwanza kisha akaomba msamaha. Baadaye nikamfungulia biashara nyumbani lakini haikuwa na matokeo mazuri na nikamueleza lakini akakasirika.

Kesho yake nikamueleza anifungulie lango kuu lakini akaja na akanirushia funguo. Hapo nikachukua simu yake na kuivunja, kurudi kwa nyumba sikumpata nyumbani.

"Kumsamehe naye nimemsamehe lakini pia yeye anipe mda kidogo, sioni vile tunaeza ishi naye saa hizi. Huu mwezi tu anipe ili nifikirie kama naweza rudi nyumbani." Alisema Mary bila kueleza ni kipi kilichotokea baina ya hao wawili.

&feature=youtu.be