PATANISHO: Mke wangu alisema atarudi kwangu baada ya miaka miwili

Michael alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake, bi Maggie, ambaye walikosana msimu wa Krisimasi mwaka wa 2018, na tangia siku hiyo hajawahi rudi.

"Enyewe kusema ukweli sikumfukuza kwani tuligombana na sababu ni alikuwa akitaka kwenda kwao na akaniomba fedha za kununua bidahaa ambazo nilimpea. Tukaagana akienda akae siku moja ili siku ifuatayo twende kwetu." Alisema Michael.

Pilka pilka ya kumpa fedha akadai haitoshi na aliomba niongeze elfu moja mia tano ili iwe elfu tatu na mia tano. Akaniambia hataenda nazo kwani hazikutosha na akanirushia fesha kwa meza na kusema nielekee kwao. Aliondoka na kurudi kwetu baada ya siku kama nne. Kumuuliza aliniambia kuwa juu sikuenda kwao pia yeye ana kwao ambapo anaweza pumzika na atosheke." Aliongeza akisema mkewe alidhibitisha kuwa hatorudi kwao kabla ya miaka miwili.

Nilitoka nikaenda kesha na kurudi nilipata ameondoka na akasema atarudi baada ya mika miwili.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili na wamejaliwa watoto wawili ambao mkewe aliondoka nao.

Maggie alidhibitisha kuwa alimkasirikia bwanake na kuwa amekuwa na mazoea na pia anataka kumtesa.

"Tuliachana 25th asubuhi na tulikuwa twende kwetu, hakufika na hakupiga simu. Sasa tarehe 28 nikarudi kwangu na tangia hiyo siku hajawahi kuja wala kusema lolote. Aje azungumze na wazazi na tutasuluhisha hayo mambo." Alieleza.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be