PATANISHO: Mke wangu alitoroka baada yangu kuchapa watoto

Leo katika kitengo cha patanisho, Bwana Richard alituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake waliotengana mwezi jana baada ya kuwachapa wanawe kwa maana hawakuwa wanakula.

Baada ya kuwachapa, mke wake alikasirika na kukusanya virago na kwenda.

"Ilikuwa Jumamosi iliyopita nilirudi nyumbani nikampata mke wangu akipiga gumzo na rafiki zake kwa nyumba alikuwa amewaekea watoto wangu chakula lakini hana shughuli ya kuwalisha

Nilikasirika na nikawachapa kwa kuharibu chakula kwa maana walikuwa wamemwaga chakula kila mahali, baada ya kuwatandika mke wangu alikusanya virago na akaenda kwa ndugu yake

Nimeongea na wazazi wake na hata ndugu zake wakaniambia amesema hataki mambo yangu." Alieleza Richard.

Mkewe Richard alipopigiwa simu alikuwa na haya ya kusema;

"Richard amekuwa na mazoea. Kuna wakati kifungua mimba wangu akiwa na miezi nne alimchapa hadi akamuuma hadi leo ana alama ya jinsi alimuuma akiwa mdogo hata akiwa miezi sita alikuwa anamchapa

Mimi sitaki kuongea na yeye si kuna siku ataua watoto wangu, si mara ya kwanza wala ya pili kufanya kitendo hicho, Jumamosi baada ya kumchapa mwanangu na hata kumuweka alama shingoni

Alitoka baada ya kumchapa alikuja hadi nilipokuwa akanisaba kofi."

Bwana Richard alikiri na kusema kuwa hawezi kuua watoto wake, pia alisema kuwa alienda kwa mhubiri na kumwambia ana shida

Naye mkewe alisema kuwa amempa muda wa kubadilika ilhali hajabadilika.

Kwa uhondo zaidi tembelea mtandao wetu wa kijamii wa youtube.