PATANISHO: MKe Wangu Alitoweka Nyumbani Baada Ya Kunituma Sabuni

Reuben mwenye umri wa miaka 29, aliwafurahisha wengi wakti alipofichua kuwa mkewe Salima mwenye umri wa miaka 24, alitoweka nyumbani mwao baada ya kutumia ujanja wa kumtuma dukani akanunue sabuni.

Haya yalitokea katika kitengo cha patanisho siku ya alhamisi baina ya wanandoa hawa wawili ambao wamekuwa pamoja kwa miaka mitano na ambao wamejaliwa watoto wawili.

"Ilikuwa Novemba mwaka uliopita ambapo tulikosana na mke wangu, baada ya kuishi kwa miaka mitano ambapo nlimsaidia kibiashara lakini mwishoni mwa mwaka uliopita alipoanza kuinuka kimaisha ndipo alipoanza maneno maneno na tuliposhauriwa na babake bado alirudia makosa ambayo ilikuwa mpango wa kando. Baadaye alitoweka nyumbani baada ya kunituma sabuni na niliporudi nilipata mlango wazi mkononi nikiwa na sabuni huku akimuacha mtoto shuleni." Alijieleza Reuben.

"Tuliamka vizuri siku moja, tukagombana kidogo, kuhusu biashara yangu lakini iifika ni mambo ya fedha nlizokuwa nazo ananishuku kuwa napewa fedha na wanaume humo nje kama alivyokuwa akishauriwa na marafikize." Alisema bi Salima.

Kulingana na Reuben mkewe alikuwa anapokea ujumbe masaa ya usiku jambo ambalo halikumfurahisha.

Bi Salima mwishowe alisema kuwa atarudiana na mumewe akiwacha tabia za kumpiga au za kumshuku ki ndoa.