PATANISHO: Mke Wangu Aliwacha Mtoto Wetu Mashambani Na Kutoweka

patanisho... (1)
patanisho... (1)
Derick 27, alitumia Gidi na Ghost ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Medrine mwenye umri wa miaka 25. Kulingana naye, wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minne na wamejaliwa mtoto mmoja.

"Mimi nilitoka tu nyumbani nikamuacha akiwa mzima na bila shida yoyote nilipokuja Nairobi kutafuta kibarua.

Akanipigia simu kuniambia kuwa nimefurahia kuwa nishafika nilikotaka, mda mchache akaniambia mtoto ni mgonjwa na nimtumie fedha za hospitali nikakopa nikamtumia.

Nikapata habari kuwa mtoto amezidiwa na hakumpeleka hospitalini, hapo nikapigia mama yangu nikamueleza yaliyotokea na hapo akamchukua mtoto na kumpeleka hospitalini, hapo mke wangu akapata nafasi na aliondoka nyumbani. Hapo ndipo niliskia kuwa ameondoka na kuuza kila kitu kwa nyumba. Tangia siku hiyo hatujaongea na sijui aliko hadi sasa." Alijieleza bwana Derick.

"Mimi niliona maisha inaendelea kuwa ngumu na baada ya mamake kumchukua mtoto hapo nikaamua kutoka nyumbani nikatafute kazi. Sikuuza chochote kama anavyo sema kwani niliwacha kila kitu bali ni vyombo tu vya jikoni nilivochukua."

Alisema bi Medrine akiongeza "Sasa nampenda tena sana."

Skiza uhondo kamili.

&feature=youtu.be