PATANISHO: Mke wangu alizua vurugu baada ya kunipata nikipika kazini

Moses aliomba kupatanishwa na Boss wake akisema kuwa alimkosea sana na kubeba virago vyake na kuondoka.

Nilikuwa nafanya kazi Kakamega na tukapata matanga nyumbani na nikamtumia fedha za kuhudhuria.

"Bosi wangu akanikubalisha kwenda nyumbani na kadhalika, sasa kufika kule nikaamua kupikia wafanyikazi wenzangu na mke wangu aliponipata pale akazusha eti kuwa sifai kufanya kazi kama zile." Moses alisimulia.

Anasema tangia pale bosi wake hajawahi muitia kazi na angependa kurekebisha hayo yote.

Alipopigiwa simu bwana Sammy alikiri kuwa yeye ni mcha mungu na kuwa alimsamehe Moses kitambo sana ila yeye ndiye alisahau.

"Kazi ikipatikana nitamuita kwani hatukupigana ila shida ilikuwa kati yake na na mkewe. Kwa site lazima kila mtu apike na hakuna mtu amekuja na mke wake. Sasa mtakosa kula kwa sababu hakuna mke wake?" Alisema bwana Sam.

Isitoshe Sam anasema kuwa kisa hicho kilitokea baada ya kufanya kazi pale kwa siku tatu pekee.

Sam aliongeza,

"Mimi naweza kumwambia ajikaze asifuate mambo ya mabibi kwani kazini mambo hayafanyiki kama nyumbani."