PATANISHO: Mke Wangu Amekuwa Akiniyima Haki Ya Ndoa

Nicholas alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Bi Felistus.

"Nilimuoa mke wangu mwaka wa 2007 akiwa kama mke wa pili ambaye nilimchukua akiwa na mtoto mmoja. Sasa ilifika wakati mke wangu hakuwa anataka mambo ya kufanya mapenzi. Nimejaribu kumtuliza hata nikamtumia marafiki zake na familia yake ili nione shida ilikuwa gani. Sasa alikuja akarekebisha kisha akarudia mambo yale yale ya kuninyima haki ya ndoa.

Sasa ilifika wakati nikapata ajali kwani nilikuwa nafanya kazi ya matatu na hapo nikawekwa chuma kwa mguu. Sasa hata baada ya chuma kutolewa bado mke wangu hataki tushiriki mapenzi na sielewi shida ni gani. Nikimguza anakasirika akidai kuwa amechoka." Alieleza Nick akidai kuwa hashuku kama mkewe ana mpango wa kando.

Mkewe hakujibu simu zetu kwani pia yeye ni shabiki wa redio Jambo.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be