PATANISHO: Mke Wangu Ana Wivu Wa Mapenzi Hataki Nizungumze Na Wanawake

Mercy alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe ambaye walikosana takriban majuma mawili yaliyopita, jambo ambalo lampatia mawazo chungu nzima kwani hana amani.

"Nilikasirika kidogo baada ya mume wangu kunipiga kwa kuchelewa kutoka kazini kwani nilikuwa nafanya biashara. Nilipotoka kazini sikumpata na hapo nikatoka kwenda kununua chakula nikampata akioga na hakunizungumzia, mda mchache baadaye akanichapa akidai kuwa nilikuwa nimetoka umalaya hata bila kuniskiza akidai nilikuwa nimebeba nguo zangu.

Hapo nikakasirika sana nikaelekea kwa kituo cha polisi kuripoti kisa hicho na nikafunga nyumba kesho yake naye akaondoka kwani nyumba ilikuwa yangu. Tangia siku hiyo huwa hataki kuzungumza nami."

Alieleza Mercy aliye na miaka 31.

Wawili hao bado hawajajaliwa na watoto.

Alipopigiwa simu bwana Frankline alieleza, "Tutazidi kusumbuana hadi lini kila wakati unashinda ukisema hivyo kisha mambo yanatokea. Mercy ana tabia ya kunikazia maisha anadhani nazungumza na wasichana, akiona nambari ya wasichana kwa simu yangu anafuta hadi ana tabia za kuwapigia wateja wangu na kuwatishia na kuwatusi, ana wivu wa mapenzi lakini hataki nishirikiane na wanawake."

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be