PATANISHO: Mke Wangu Anafaa Atulize Boli Atakuja Kupeana Pasi Kwa Opponent

Dickson alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Maureen.
Tulikosana na mke wangu zaidi ya miaka miwili iliyopita. Alipotoka nyumbani alidai ameelekea nyumbani kwenda kuona wazazi wake lakini aliporudi kwa dadake tulikosana baada ya kunipata na mpango wa kando.

Baadaye tulizozana kidogo na nikampiga. Hapo akakasirika na kutoka kwangu baada ya miaka minane.

Wawili hao wana watoto wanne lakini mmoja aliaga dunia.

Dickson alikiri kuwa amekuwa akimfuatilia Maureen ambaye ni mke wake wa pili na akagundua kuwa amekuwa akiishi na wanadada wengine watatu.

Aliongeza kuwa mkewe mkuu alipatana na Maureen na akamhakikishia kuwa atarudi nyumbani siku moja, ila hakusema ni lini.

"Maureen anafaa kujua kuwa azunguke dunia akijua kuwa uwanja ni mdogo atulize boli atakuja kupeana pasi kwa opponent." Alimpa mkewe mawaidha ya mwisho.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be