patanish.2018

PATANISHO: Mke Wangu Hupotelea Kwa Kichaka Kila Ninapoenda Kwao

John aliomba apatanishwe na mkewe Teresia ambaye alitoroka mwaka jana mwezi wa nne pamoja na watoto watatu. Kulingana na John amejaribu kumrudisha nyumbani bila mafanikio.

“Tulikuwa tunazungumza tulipoenda kesi kwao na tukakubaliana kuwa atarudi mwezi wa nane.

Siku kadhaa kabla ya kufanya uchaguzi akanieleza kuwa nimpe mda ili afikirie na mara ya mwisho kuskia kutoka kwake alidai kuwa ameamua kuishi kwao na kuwa ana mipango ya kujenga. Akiskia nimewasili yeye hutoroka kwa kichaka mimi nikizungumza na watoto naondoka.

Hakuna kitu tulikosania kwani nielekea mazishi tukiwa tumewachana vizuri. Kurudi nikaelezwa kuwa nafaa nijipange mambo ya kujipikia kwani mke wangu amesimamisha gari na amebeba kila kitu nyumbani.” Alijieleza John.

Kutafuta usaidizi kwa askari, wakanieleza kuwa nafaa kuekelea mbuzi kwa meza ili wanisaidie. Siku kadhaa baadaye alipatikana akiwa amesafiri hadi nyumbani.” Aliongeza akifichua kuwa wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na miwili.

Bi Teresiah naye alitumia ujanja wa kukata mawasiliano yetu.

Pat uhondo kamili.

Photo Credits: victor TKO imboto

Read More:

Comments

comments