PATANISHO: Mke wangu ni kama amechukuliwa na mchina

Zack, 31 aliomba apatanushwe na mkewe bi Mary, 27, akiomba ndoa yake iokolewa kwani walikosana na mkewe akabeba kila kitu na kuhamia karibu na kazini kwake.

Isitoshe aliwashangaza watangazaji, Gidi na Ghost aliposema, "Jana karibu nijitoe uhai na wakti nilikuwa ninywe simu, dadangu ambaye sijazungumza naye mwaka mzima akapiga simu."

Zack anadai wamekuwa wakigombania mambo madogo kama; mtoto akikosa kuoshwa au kuoshwa mara moja tu kwa wiki.

Isitoshe, anadai juzi mkewe alimpa maji ya kunywa na kikombe kichafu ambacho mle ndani kulikuwa na mchele.

Hapo tuligombana na kesho yake aliporudi nyumbani kutoka kazini alipata mkewe ameondoka na watoto na kubeba kila kitu kwa nyumba." Aliongeza.

Alipopigiwa simu, bi Mary kwa hasira tele alisema,

"Nilimpigia simu asubuhi na nikamwambia akiwachwa awachike!"

Aliongeza,

Mwambie sister yake amtafutie mke mkisii mwenzake, huyo mtu ni stress na hataki nifanye kazi ila hata chakula hawezi nunua. Nikipata kazi anadai nina wanaume humo nje na katika harakati ile amenipasulia simu kadhaa." Alisema Mary.

Mary alipopewa fursa ya kuzungumza na aliyekuwa mumewe alisema amechoka na Zack na akitaka bwana atamrudia jamaa aliyemuoa kitambo.

"Mbona ulikuja kazini kudai kuwa nimeiba ma cable za stima na karibu nifutwe kazini? Ambie Salome akutafutie bibi!" Alifoka kabla ya kusitisha mawasiliano kati yao.

Aliniambia kuwa simu yake ni mwanaume mchina alimnunulia na alikuwa anamtongoza na alikuwa anampigia simu kila usiku na nikakasirika na nikapasua simu.