PATANISHO: Mke wangu ni wale wamelelewa kama paka ya duka

Bwana Idi, 41, alituma ujumbe wa patanisho akiomba apatanishwe na mkewe bi Yvonne, 38, na kusema kuwa ndoa yao ya mwaka mmoja inyumbayumba.

"Nimekuwa na mwanamke ambaye nampenda na tumeishi vyema lakini juzi ameanza kuleta vitisho kuwa anataka kwenda nyumbani. Sikuelewa mbona na pia akasema anashuku kuwa ana uja uzito na kwenda hospitalini akathibitisha." Alisema Idi.

Aliongeza,

Hapo akashtuka alipogundua ana mimba na shida ya mke wangu ni wale watoto wamelelewa kama paka ya duka, akisema anataka hii anapewa na akikosa ni vurugu."

Idi anasema mamake Yvonne alipoaga, msichana aliwahi jaribu kujitoa uhai mara tatu baada ya kusombwa na mawazo lakini anaponea.

Juzi aliniambia nitafute nyumba na nilipopata tena hataki kuishi kule na isitoshe anataka kwenda kwa babake ampatie elfu saba ili akatoe ile mimba.

"Sina shida na yeye kwani kuna wakati yeye hurusha maneno na mambo madogo anafanya yawe makubwa." Alisema Yvonne huku akimwambia mpenziwe kuwa asiwe na wasiwasi kuwa ataavya mimba.

Kwa upande wake, bwana Idi alijitetea akidai kuwa hana na hapendi mambo mengi.