Patanisho.Moses alituma ujumbe kupatanishwa na mkewe aliyepata mtoto nje ya ndoa

NA NICKSON TOSI

Leo katika patanisho, Moses mwenye umri wa miaka 30 kutoka Katani Syokimau, ambaye ni dereva wa magari ya uchuguzi wa umma, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mkewe ambaye alidai alipata mtoto nje ya ndoa pasi na ufahamu wake.

Moses alisema amekosa penzi la mkewe ambaye alikuwa amekaa kwao miaka miwili na alikuwa amejaribu kuoa bila kufanikiwa katika ndoa hizo.

'Mimi nafanya kazi hapa Nairobi kama dereva na mke wangu amekuwa akiishi nyumbani, mke wangu aliitisha sana kuja Nairobi kunitembelea na kama mume nikamruhusu aje, kawaida kama mwanamume yeyote akitembelewa na mkewe, lazima mtashiriki tendo la ndoa. Nilishangaa wakati ambapo alirejea nyumbani na kwa muda mfupi nikapata ripoti kuwa amejifungua mtoto, tulizozana na mke wangu. Mke wangu wa miaka sita, mama Mitchelle alifunga virago na kuondoka.  

Alipopigiwa simu mama Mitchelle alikuwa na haya ya kusema.

Mitchell alimkashifu Moses kwa kile alisema wakati alipokuwa Nairobi alianza kumdharau na hata kumpatia mpango wake wa kando simu azungumze naye,

Nilikuwa nakupigia simu na unampatia mpenzi wako wa kando Nairobi. 

Nikipiga simu ulikuwa unasema niombe huyo mkeo wa Nairobi pesa ilhali mimi niko huku nyumbani na watoto na hatuna chakula kwa nyumba ,alisema Mama Mitchelle.

upande wake Moses alipinga madai hayo akisema wakati alipokuwa anatuma pesa za kujenga nyumbani, mkewe alianza uhusiano wa kimapnzi na fundi hadi akapata mimba.

alikuwa anatuma shilingi mia 500 , na tuna watoto wawili, hapo na maisha ya sasa huezi kujikimu kivovyote vile ,alisema Mama Mitchelle.

Mama Mitchelle alisema atarejea kwa ndoa iwapo Moses atawacha madharau.

Rose hakuna siku nitakuonyesha madharau, na kila jambo ambalo limefanyika kati yetu nimeliweka katika kaburi la sahau, lakini nakuomba uwe ukishika simu tafadhali, naomba urejee nyumbani tulee watoto wetu.

Rose wajua nakupenda sana, nakupenda kama katunda kadogo kwa jina passion fruit,alisema Moses.

Mimi nakupenda lakini una madharau sana, nitarudi baada ya mwezi mmoja ili tuendeleze ndoa yetu na tulee watoto, alisema Rose.