PATANISHO: Mpenzi wako nikama alikutumia na kukutenga - Gidi

patanisho (1)
patanisho (1)
Anita alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mpenziwe bwana Timo, ambaye walikuwa wameanza mipango ya kufunga ndoa.  Anasema walijuana Novemba na Disemba ndipo walianza kuchumbiana na Januari tayari wameanza kupambana.

"Mpenzi wangu anaishi na rafiki yake ambaye aliniomba hela ambazo alikataa kulipa, sasa siku moja kwenda kumtafuta kule walikataa kufungua mlango na nilipoingia hadi chumbani nilipata nduguye Timo na msichana mwingine kitandani." Alieleza Anita.

Anita mwenye miaka 23, aliongeza,

Hapo Timo alinipigia simu akipiga kelele kuwa nimewaaibisha ndugu yake na mpenziwe na akakataa msamaha wangu.

Hata hivyo kulingana na upekuzi wa Gidi ni bayana kwamba huenda yule Timo ndiye aliyekuwa na mpenzi mwingine ila akamuita nduguye aje kitandani ili Anita adhanie kuwa ni mpenzi wake.

Baada ya bwana Timo kukatisha mawasiliano kati yetu Gidi hakuwa na budi ila kumpa Anita ukweli. "Kuongea ukweli huyo jamaa alikutumia na kukutenga, hata hizo fedha ulizokopesha rafikiye wachana nazo mungu atakupa zingine."

Je ni mawaidha yepi unaweza kumpa bi Anita?