PATANISHO: Mteja wangu ndiye aliniharibia ndoa

Fred alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Rael ambaye walikosana miezi miwili iliyopita.

Mimi huwa mtu wa bodaboda na kuna alikuwa ananipigia ili nimpeleke sokoni kila siku, ikawa ananipigia simu hadi usiku nimuendee. Mke wangu ambaye anamjua akaanza kunung'unika akisema kuwa tuna uhusiano.

Siku moja yule msichana akanipigia simu na mke wangu kitu saa mbili akanipigia simu akisema kuwa ameondoka na kuwa nafaa kubaki na yule mwanadada ninayempenda. Aliongeza akisema kuwa hakuwa na uhusiano wowote na yule mwanadada.

Wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja katika ndoa ya miaka miwili.

Alikuwa na rafiki ambaye alikuwa anamchukua na boda kitu saa kumi usiku na hapo nikaamua niondoke. Nikama walikuwa wanaelekea mahala kwingine kwani saa kumi wanaenda wapi? Aliuliza Rael akisema kuwa kila alipouliza alikuwa anagombanishwa.

Bwana Fred naye alikiri kuwa amewachana na yule mteja kwani amegundua kuwa anamharibia ndoa yake.

Rael alikubali msamaha wa bwana yake na kukiri kuwa atarudi nyumbani ili walee mtoto wao.

&feature=youtu.be