PATANISHO: Mtu akiniita aninunulie pombe nitamshtaki!

Bwana Moses aliomba apatanishwe na mkewe mpendwa bi Rose akisema ameshindwa na juhudi za kumrudisha mpenziwe nyumbani.

Kulingana na Moses, wawili hao walikosana miaka mitatu iliyopita lakini hadhani mkewe amepata mwingine kwani "Kuna wakati nilitaka kujenga nyumba na alikuja kunisaidia kujenga."

"Niliambiwa kwamba yuko Nairobi kikazi lakini nikimuuliza huwa hanielezi aliko na yeye husema kuwa hana kazi." Alieleza mzee Moses.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka ishirini na mitano na wamejaliwa na watoto watano.

Mzee Moses ana umri wa miaka 55 huku mkewe akiwa na miaka 45.

Alipopigiwa simu mama Rose alikiri kuwa anamtambua bwana Moses kama mumewe kwani yeye humtembelea mara kwa mara.

Unajua sio rahisi mtu akae miaka ishirini na atoke kwa ndoa, kwani nilishatoka. Nina watoto lakini huwa naenda kwake lakini ana shida moja, kama mnaweza msaidia na mambo ya kuwacha ulevi ni sawa. Alieleza Rose.

Unajua akienda ulevi mimi ndio huchapwa na isitoshe mambo ya ulevi ndio ilifanya akapoteza kazi. Tuna watoto wako chuo kikuu na shule ya upili. Aliongeza.

Akijitetea, Moses alisema alimpiga tu mara moja lakini maneno ya kazi ni kuwa alipoteza kazi baada ya mbunge aliyekuwa akimfanyia kazi alipoteza kiti.

Sahii natangaza kuwa nimerudi kwa kanisa na nimeenda jumapili tatu katika kanisa la Malaba PEFA church, na mtu akiniambia twende tukanywe pombe nitamshtaki." Alijitetea bwana Moses.