PATANISHO: Mume amekataa kukubali watoto wangu

Bi Jacky alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Godfrey, huku akidai kuwa ana mawazo mengi mno. Chanzo? Mumewe alimuoa na watoto wawili lakini hataki kukubali mmoja kama mwanawe.
Mimi nilipata watoto wawili wa kike nikiwa kwetu na wakati alitaka tuoane nilimweleza nina watoto na nikauliza kama atakubali kunioa na watoto. Akasema hana shida lakini alirudi akasema kuwa atamchukua mtoto wangu mdogo na mkubwa akabaki na mamangu. Alisimulia Jacky.

Aliongeza;

Baadaye alipelekwa kwa baba yake na alikuwa anateseka hadi siku moja akakimbia na kuja kwangu na pikipiki usiku.

Kumuuliza alisema kuwa mama wa kambo anamtesa lakini huyu mume wangu anakataa kumchukua akisema kuwa babake ana pesa kumshinda.

Isitoshe, wawili hao hawafanyi mapenzi kwani hata humaliza miezi miwili bila kushiriki mapenzi.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minane na wamejaliwa mtoto mmoja pamoja. Akiongeza, Jackline alisema kuwa wawili hao hawana amani kwa nyumba.

Kuna siku nilikupata na mwanaume fulani ukaniambia mlikuwa busy, sijui mnafanya nini na mlikuwa mme egeza gari kando, mlikuwa mnafanya nini? Aliuliza Godfrey.

Kuna siku nilikuwa na urafiki wa nje na nikaona niko sawa lakini nikirudi nyumbani nashindwa kufanya kazi sijui shida ni ipi.