PATANISHO: Mume nilimbadilisha sahii anafanana na MCA

patanisho.000
patanisho.000
Bi Agnes Njeri ndiye aliyeomba kupatanishwa huku akidai aliskia fununu kuwa mumewe bwana Basil Wafula ana mipango ya kurudi kwao Uganda. Njeri ambaye anasema amesombwa na mawazo, anafikiria kujitia kitanzi.
"Huyo mwanaume nilikuwa nampenda sana na tulikuwa tunaishi Juja farm na maisha yakawa ngumu kwani hatukuwa na vibarua na nyumba ilikuwa karibu kufungwa." Alisema Agnes.

Aliongeza,

Nikamwambia mume wangu angoje nikule fedha za chama ili tufanye biashara ya kuuza vitenge. Siku moja niliambiwa kuwa kuna msichana ambaye hufua nguo na kuna wakati hulala kwa nyumba.

Nilipomuuliza akakasirika sana na mchana huchukua simu zangu lakini usiku huwa hajibu. Sielewi na vile pamoja tumetoka mbali na kama hana fedha huwa namsaidia.

Njeri anasema isitoshe laini ya simu ya Basil aliyobaki nayo huwa anapigiwa simu na wanawake huku wakimtusi.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili na wamejaliwa mtoto mmoja na tayari Njeri ana mimba ya miezi mitatu.

Isitoshe nikimwambia anasema kuwa mimba ni ya babangu ama ndugu yangu. Gidi huyu mwanaume nilimpata akifanana na mwizi na nikamuosha na kumtengeneza na sasa anafanana MCA."

Agnes anasema kuwa watu walishangazwa na hatua yake kumuoa Basil wakidai yeye anafaa kuolewa na mtoto wa rais. Hapo Agnes aliwaambia kuwa mapenzi sio pesa na kuapa kumbadilisha mumewe.

Alipopigiwa simu bwana Basil alikiri kuwa hamtesi mkewe.

Agnes alifichua kuwa wanawake watatu waliwahi mpigia simu huku wakimtusi na hapo hangeweza kujitetea.

Kitu ilifanya niwache kumpigia simu ni kuwa aliwahi niambia ameolewa na hapo nikawacha." Alisema Basil akidai kuwa hafai kuwa na wasiwasi na bado anamngoja huko Juja farm.

Nakupenda kama chipo! Agnes alimwambia mumewe pindi tu alipogundua kuwa yuampenda pia.