PATANISHO: Mume wangu akiapa kula chakula changu nitamrudia

Bob collymore and uhuru kenyatta
Bob collymore and uhuru kenyatta
Morris, 26, aliomba apatanishwe na mkewe, mama Max, 22, ambaye walikosana mwaka jana alipompata akimtongoza mama mdogo

"Unajua baba yangu alikuwa na wanawake wawili na nilikuwa very close na mke wa pili kwani alikuwa rika langu. Tulikuwa close sana na kuna wakati bibi alipata tukizungumza na alidhani kuwa namtongoza na hapo akatoweka na kuniwachia watoto." Alisema Morris.

Aliongeza kuwa kuna wakati alikuwa ana kula kwake na kuna wakati alikuwa anatoka kwake usiku jambo ambalo halikumfurahisha mkewe.

Morris aliongeza,

Nikimpigia simu yeye huniambia niende nimtafute yule mama mdogo. Nashtuka kwani sikuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.

Wawili hao wamejaliwa watoto wawili.

"Mbona ulimpenda mama mdogo kuliko mamako mzazi? " Mama Max alimuuliza.

Akijitetea, Morris alisema kuwa mkewe na mamake mzazi wana tabia ya kupika polepole au kupika wakiwa wamechelewa na hilo lilimfanya kukimbilia mama mdogo.

Imefika wakati nikipika chakula hataki anaenda kula kule akisema kuwa yule ndiye anayepika vyema. Alijitetea Morris.

Mama Max alisisitiza kuwa atarudi kwa mumewe kama Morris ataapa kuwa atakula chakula chake kwani hilo ndilo shida kuu kati yao.