PATANISHO: Mume wangu akilewa hutishia kuniua na nikaamua nikimbie

Michael alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Florence.
"Tumekosana kwa kipindi cha miezi mitano na kulingana naye malalamishi yake ni kuwa nabugia pombe sana. Nilikuwa safarini baada yetu kukosana ili nimpe nafasi na kule mawasiliano hayakuwa mazuri nikiwa nyumbani.

Niliporudi nilipata amehama na nilijaribu kumfuatilia na tukajaribu kupatanishwa na wazazi na kusema pombe ndio inatutenganisha." Alieleza Michael akisema bado hajawacha pombe.

Najaribu kuwacha lakini kila ninaposombwa na mawazo hubidi naenda kutoa lock. Aliongeza.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka 19 na wamejaliwa watoto wawili.

Alipopigiwa simu bi Florence alisema kuwa anahitaji mda kwani anapitia hali ngumu.

"Nipe mda nawe pia uchukue mda utafakari. Msamaha nitakupa lakini kuna yale maadili tunafaa tuketi chini tuzungumze." Alisema Florence.

Mume wangu anakunywa sana lakini imepindukiwa kuanzia miaka tisa iliyopita na nimejaribu kuzungumza lakini sioni mabadiliko.

Isitoshe, Florence alisema kuwa mumewe akilewa huwa na fujo tele na ilimbidi ajitenge kwani ana majukumu ya kulea watoto wake.

&feature=youtu.be