Patanisho: Mume wangu aliambia wajomba wangu nirudi kwake 2020

Amos alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Faustine ambaye alimkosea kwa kujihusisha na mipango ya kando.

Isitoshe, kulingana na Amos, Faustine alisema kuwa licha yao kuwa kwa ndoa ya miaka saba, mtoto waliyefanikiwa pamoja alikuwa wa mpango wa kando.

"Mimi nilikuwa nafanya kazi Nairobi, kisha baadae nikatoka kwa ajili mke wangu bi Faustine alikuwa na mipango ya kando na nikashindwa kufanya kazi. Tetesi zilikuwa eti mke wangu anasumbua kule nyumbani na anatembea tembea vibaya." Alisema Amos.

Aliongeza akisema, sasa venye nilikuja nyumbani, nikajinyamazia na nilipofuatilia hayo mambo nikapata alikuwa na mpango wa kando. Isitoshe, nikapata ujumbe kwa simu jamaa akidai kuwa mtoto wao ni wake, licha ya wawili hao kuwa kwa ndoa ya miaka saba.

Mwishowe mkewe alikiri mtoto ni wa ule jamaa na hicho kilimkasirisha na hapo alimpiga na mkewe akaondoka.

"Kila kitu mtoto ni wangu, ananinifanana na hata nimekuwa nikimsomesha mwenyewe." Alieleza bwana Amos.

Si wewe ulinipea mwaka? Siwezi rudi sahii. Ulipigia mjomba wangu simu ukamwambia nimepea huyo msichana wenyu mwaka mmoja atulie." Alijieleza Faustine huku akidai atarudi kwa Amos, 2020. Vumilia tu huo mwaka mmoja." Aliongeza.

Pata uhondo kamili.