PATANISHO: Mume wangu alinipiga kwa chupa na kunitupia mavazi chooni

Bwana Collins alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe, mama Ken ambaye walikosana mwezi wa nne na akarudi nyumbani kwao.

"Ilikuwa ni mambo na ulevi kwani alikuwa amenikanya niwache ulevi na nisipojirekebisha atarudi kwao.

Hata sikuwa nimekunywa hiyo siku sanaa kwani nilikuwa nimekunywa chupa mbili pekee za beer, kufika kwa nyumba nikamwambia anipashie chakula nile na marafiki zangu ili warudi nyumbani." Alieleza Collins akidai kuwa mkewe alikasirika na akatoka nje ambapo waligombana kisha akaondoka.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka tisa na wamejaliwa watoto watatu.

Huwa nampigia simu lakini huwa haoneshi interest hataa.. Isitoshe nyumba yangu ya nyumbani iliibiwa kwani hamna anayeishi huko." Aliongeza.

Nimemvumilia sana mume wangu maneno ya pombe na bangi ndio anapenda kutumia, cha pili haheshimu familia yangu.

Hata watoto wakimuona wanamuogopa kwani anapenda vita sana. Amenichomea nguo zangu mara kama tano, amenikata kwa panga na isitoshe akanitupia nguo zangu kwa choo." Alijieleza mkewe akidai mateso aliyopitia ni mengi.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be