PATANISHO: Mume wangu alinitenga baada ya kukataa kuavya mimba

Anne Jepkorir alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe akidai kuwa ana watoto wawili na kuwa anapanga kuwapeana baada ya maisha kuwa mazito.
Mara ya mwisho kuzungumza naye alisema anaenda Nairobi lakini hakuwa huko na nikimpigia hakuwa anashika simu. Alisema Anne

Tuna watoto wawili, baada ya kupata mtoto mmoja nikashika mimba ya pili baada tu ya miezi mitano.

Nikama hakuwa anatarajia kwani kuna siku alikuwa anadai nitoe mimba na nikakataa.

Hapo alikasirika na kunieleza kuwa sifai kumhesabu ndani ya maisha yake, hapo nikamnyamazia na nikaondoka. Baada ya kurudi miezi tisa baadaye alianza kulia alipomuona mtoto kwani aliamini ni wake na akapata machungu kuwa karibu aue mwanawe." Alieleza Anne.

Bwanake alikatisha mawasiliano nasi pindi tu aliposkia sauti ya mkewe.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be