PATANISHO: Mume wangu alinizuia kwenda na mtoto anaye nyonya

Robert ambaye mkewe aliondoka miezi miwili iliyopita na kumwachia mtoto wa miezi saba, alituma ujumbe akiomba apatanishwe, na ndoa yake iokolewe.

Mke wangu aliondoka tarehe 13 mwezi wa saba na hadi wa sasa hajarudi. Aliniwachia mtoto wa miezi wa saba anayenyonya na sasa hanyonyi Kwani mke wangu bado yuko nyumbani. Alieleza Robert.

Kulikuwa na ugomvi wa nyumba kwani mke wangu ilifika mahali akakataa majukumu ya nyumba kwa mfano hakuwa anataka kupika na akaondoka. Tulizungumza naye akaniambia atarejea Septemba.

Wawili hawa wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili na wazazi wanamfahamu Robert ila bado hajalipa mahari.

Licha ya maelezo hayo, bi Emma alipopigiwa simu alisema mumewe alikuwa anamchapa na hilo lilipelekea yeye kuondoka.

"Umepeleka radio jambo ndio? Hujanipigia simu na Huko Siwezi zungumza.
Kwani vitu ulifanya hukujua utajuta?" Aliuliza mkewe kabla ya kusitisha mazungumzo Kati yetu.

Hata hivyo, Robert alikiri kuwa alimpiga mkewe na ndio maana akaondoka.

Ni poa umeomba msamaha lakini unipe mda kwani bado naumia.

Emma alizidi kueleza,
Si ulichukua mtoto ukapatia mama wako ningefanya nini? Nilitaka kuondoka na mtoto na akaniambia kuwa sikuja kwake na mtoto na nilipoendelea kumwambia namtaka mtoto wangu alitishia kunichapa.
Mimi nataka anitapatie mtoto na roho yangu ikitulia nitarudi.