PATANISHO: Mume Wangu Amenifungia Kwa Nyumba Kama Zero Grazing

Hapo jana, Bwana Isaac 34, aliomba apatanishwe na mkewe Joyce, 32, ambaye akiri aliondoka na kumuacha baada yake kwenda mazishi ya shangazi yake.
"Mimi nilikuwa kwenye mazishi halafu nikaskia mama mke amenipigia simu huku akiniarifu kuwa msichana wake ametoweka na amerudi nyumbani. Hapo nilishtuka na kumpigia bibi yangu simu na hakuna alilosema kwani alisema hakuna kitu kibaya. Nimezungumza naye baada ya matukio hayo lakini akaniarifu nimtumie nauli lakini nikaona kwanza nitumie patanisho ili tuelewane."

Alijieleza bwana Isaac ambaye pamoja na mkewe wana watoto wawili wasichana, katika ndoa ya miaka sita, huku akiongeza kuwa mkewe alienda nao kwao.

Alipopigiwa simu bi Joyce, alidai kuwa alishindwa kuvumilia shida, kichapo na maneno mengi pale nyumbani.

"Alikuwa na tabia ya kuoa wake kadhaa lakini wanamtoroka mwingine akampiga na kumng'oa meno na licha ya hayo yote bado amekuwa akinipiga na kati ya wote mimi ndiye nimevumilia sana, nimefungwa hapo kama zero grazing. Hanipatii naasi ya kuenda nyumbani. Alipo enda matanga nikashukuru mungu kwani nilipata nafasi ya kutoka kwake na kuelekea nyumbani na nikachukua watoto wangu."

Alisimulia bi Joyce.

"Vile nampenda mimi huwa na wivu kiasi, aki ndugu yangu sijui huwa namna gani." Akajieleza Isaac kabla ya bwana Ghost kumlisha kiapo.

&feature=youtu.be