PATANISHO: Mume wangu amezaa na wake wawili nje ya ndoa

Titus na mkewe mama Peter akisema jana alifika nyumbani na kupata tu watoto huku mama watoto akiwa ameondoka.

"Wakati alitoka kazini alichukua nguo zake, akanunuliwa watoto wetu wawili chips na akasema kuwa ameenda kutafuta nyumba na akaondoka. Nilimpigia mamangu simu, mke wangu anaambia watu wengine kuwa sifai kumpigia simu." Alieleza Titus.

Anadai kuwa aliwahi muuliza mkewe mambo ya nyumba na katika harakati ya hasira akamwambia hafurahii kuishi naye na mkewe akakasirika.

"Nilikuwa namshuku ana uhusiano na jamaa fulani rafiki yake, nilifanya uchunguzi wangu na nikagundua kuwa wana uhusiano. Kumuuliza maneno ya mbona alipata mimba kabla hatujazungumza akakasirika." Aliongeza.

Isitoshe, mkewe alisema atakujia watoto wake baada ya kupata nyumba.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka 12.

Huyu mzee amekuwa akinitishia maisha saa zingine anasema atanikata miguu. Mimi sikuwa na kazi kwa miaka mingi na sasa baada ya kupata kazi na simtegemei sasa hafurahii.

Isitoshe anataka nikae kwa nyumba." Alisimulia mama Peter.

Aliongeza,

Isitoshe aliongeza kuwa jamaa amezaa na wanawake wawili nje na huwa anachapisha watoto katika mtandao wa Facebook. Na hadi dada zake ndio hunionesha zile picha.

Licha ya shutuma hizo zote bwana Titus anasema kuwa mume anapaswa kuwa na mpango wa kando lakini mkewe hafai. Mama Peter naye alisema hana mpango wa kando lakini akimpata atakaa naye.