PATANISHO: Mume wangu ana uhusiano na wanaume na wanawake!

Karume, 37, ndiye aliyetuma ujumbe wa kupatanishwa hii leo akitaka kupatana na mkewe bi Rachel akiongeza kuwa angetaka asaidiwe mkewe arudi nyumbani.

"Nimefanya makosa kwani ndugu yake aliniletea siasa ambayo sio ya ukweli akisema kuwa mke wangu ana rafiki na anamshawishi vibaya. Eti nikimpa mke wangu fedha yeye huenda kumuonesha rafikiye na nilimueleza kuwa hizo njia anazoelekea sio bora." Alisema Karume.

Aliongeza,

Shida ilitokea tu alipojaribu kumueleza mke wake na ni mke ambaye tulijengana naye na sasa familia yangu inataka nimrudishe nyumbani. Baba yangu ananilaani akisema sitapata amani bila yeye."

Wawili hao wana mtoto mmoja na wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitano.

"Staki kuongea na huyo mtu nitakata simu kwani staki kuskia sauti yake na asijaribu kutaja Esther." Alisema mama Chelsea alipopigiwa simu.

Nilimuachia ndugu yangu awe bibi yake ananifuata fuata nini? Akipatana na wanaume ako nao akipatana na wanawake ako nao na isitoshe hata mtoto wa ndugu yake."

Mama Chelsea anasema mumewe alimpeleka kwa OCS na nikafungiwa kwa wiki mzima akidai rti nirudi kwake cha lazima.

Kwa upande wake, bwana Karume alisema amempigia mkewe magoti akiomba msamaha ila mama Chelsea anasema asipigiwe magoti yeye sio mungu.

"Achague kati ya Faith aliye zaa naye au wanawake wengine wawili wawe wapenzi wake. " Alisema Rachel akidai hii ni patanisho ya Kieleweke.