pata patanisho

PATANISHO: Mume wangu atafute mke kutoka Coast watusiane!

Cornelius alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Mary ambaye walikosana mwezi uliopita na akaenda kwao.

Patanisho: Ni upuzi tu! Mume afunguka kuhusu kuwa na mpango wa kando

Mke wangu alikuwa mja mzito na nilipoenda kumuona nikasahau simu yangu kitandani chake na kwenda kujisaidia, niliporudi nikapata ashachukua number kadhaa kutoka kwa simu.

Kurudi nyumbani nikiwa na watoto akanitumia ujumbe akisema kuwa siku zangu zimefika na alisema amempigia mwanadada fulani na nikakanusha. Pale hospitalini siku iliyofuata alipoleta yale maneno nikakasirika na nikamkorofisha.

PATANISHO: Nashuku mke wangu ana mpango wa kando

Alisema kuwa alimaliza siku mbili bila kwenda kumtembelea na alipotoka hospitalini mambo hayakuwa mazuri, na hapo wakaanza kupitana na kutusiana kwa nyumba.

Siku chache kadhaa mkewe alisema anataka kwenda nyumbani kwao na alipomsindikiza, mkewe alimpigia simu alipofika na kusema kuwa hiyo ilikuwa siku ya mwisho wao kuonana.

Nilipomuuliza mbona alisema kuwa hakutaka kuniambia anaenda kwani ningeleta vurugu na nikimpigia simu yeye hataki kuniongelesha na husema tu nizungumze na watoto. Isitoshe yeye hunitishia kuwa nikikanyanga Murang’a nitakipata. “ Aliongeza.

Cornelius aliongeza akisema yule mwanadada aliyekisiwa naye walijuana Facebook na hawakuwa wamekutana.

Wawili hao wana watoto wanne baada ya ndoa ya miaka 14.

Alipopigiwa simu bi Mary alicheka pindi tu aliposkia mumewe ndiye aliyetaka kupatanishwa.

“Kama umerekebisha tafuta mke mwingine umuoe halafu muishi na hayo marekebisho, hivo ndio mambo yako.” Alisema Mary akimwambia mumewe kuwa makosa yake ana matusi chungu nzima.

Aliongeza, Wewe kaa na shetani wako, mimi wacha nikae na mungu.

PATANISHO: Mpenzi wangu ananitenga licha ya kuahidi kunioa

“Sasa si atafute mcoasti ambaye ambaye amezoea matusi kuanzia Monday hadi Sunday kuanzia asubuhi hadi jioni, na hata majirani wanamjua.”

Isitoshe bwana Cornelius alisema anashuku mkewe anapotoshwa na polisi wenzake wakimwambia kuwa anapaswa kuita polisi kila anapopigwa hata kama ni saa saba za usiku.

Hata hivyo bi Mary alikataa katakata kurudiana na mumewe na kukata simu.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments